Mafunzo kwa Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata yaliyoanza Agosti 4, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Chato yamehitimishwa rasmi leo Agosti 6, 2025 na Mgeni rasmi akiwa Bi. Maria Ndohelo ARO Jimbo la Kaskazini kwa niaba ya R.O Jimbo la Kusini na Kaskazini Chato Ndg Abel Johnson Manguya.
Mafunzo hayo yenye lengo la maandalizi kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba mwaka huu, yanafanywa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kuhakikisha watendaji wa uchaguzi katika ngazi zote wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sheria, kanuni, taratibu, na3 maadili ya uchaguzi ili kuendesha zoezi kwa haki na uwazi.
Akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo, Bi. Maria amewapongeza na kuwashukuru waandaaji na washiriki wote wa mafunzo hayo kwa kuhakikisha mafunzo yanakamilika vizuri na kwa umahiri ili kazi ikafanyike kwa weledi.
"Kabla ya kuanza mafunzo mlikula kiapo Cha kutunza Siri, kiapo hicho kwa mujibu wa kanuni ya 8 ya kanuni ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2025, ukiukwaji wa kiapo hiki kwa kuanza kutoa taarifa za Siri ambazo tume haikukupa maelekezo ya kuzitoa maana yake utakuwa unatenda kosa la Sheria na utawajibika kwa mujibu wa sheria" amesema Bi.Maria.
Katika zoezi hilo washiriki walipata nafasi ya kuuliza maswali, kushiriki mijadala, na kujifunza kutoka kwa wakufunzi waliobobea katika sheria za uchaguzi, utatuzi wa migogoro ya uchaguzi, na mawasiliano ya kijamii.
Kwaniaba ya washiriki Bi. Zulpha Mapinda amekiri kuwa mafunzo, kiapo na miongozo waliyopewa vitawasaidia kuendesha zoezi la uchaguzi kwa ubora na ufanisi unaotarajiwa.
Mafunzo hayo yamehitimishwa Leo Agosti 6 ,2025 ambapo washiriki wamesisitizwa kutoa ushirikiano wa kutosha pindi watakapo kwenda kuwafundisha wahusika wengine watakao simamia uchaguzi ili kuboresha zoezi hilo muhimu kwa Taifa letu.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.