Mafunzo ya maafisa Ugani wa mifugo zaidi ya 60 yaliyoanza Machi 25/03/2024 yamehitimishwa rasmi leo Machi 26/03/2024 na Katibu tawala mkoa wa Geita aliyewakilishwa na
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Elfas Msenya kwa kuipongeza na kuishukuru Serikali kupitia wizara ya Mifugo na Uvuvi kuleta programu hiyo iliyowapiga msasa maafisa mifugo wa ngazi ya vijiji na kata wa mikoa ya Kanda ya ziwa Magharibi.
Dkt. Msenya amewataka maafisa mifugo kwenda kutekeleza kwa vitendo yale waliyofundishwa kwani lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo katika kupata maarifa mapya ya teknolojia na ujuzi ili wakafanye kazi kwa ufanisi na kujiamini zaidi huku elimu hiyo kupitia wao ikawasaidie wafugaji kufuga kibiashara.
"Ndugu watumishi maafisa Ugani wenzangu nawapongeza nanyi pia kupata fursa hii kushiriki mafunzo yaliyoandaliwa na wizara yetu pendwa ya mifugo na Uvuvi naamini kwa siku mbili hizi mmejifunza mada mbalimbali ambazo zitakwenda kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku na kuiinua Sekta ya mifugo, nawasihi mkayafanyie kazi kwa vitendo mafunzo haya na mkawabadilishe wafugaji wetu waache mazoea bali kupitia ninyi wakafuge kitalaamu waongeze uzalishaji kwa kufuata taratibu za ulishaji, matibabu pamoja na chanjo" Alisema Dkt Msenya.
Agnes Nicholaus ni mmoja kati ya washiriki wa mafunzo hayo akiwa ni Afisa mifugo kutoka kata ya Luchelele wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza amekiri kufurahishwa na namna watoa mada walivyokuwa wakiwafafanulia na kuhakikisha washiriki wote wanapata uelewa wa pamoja ndipo wanahamia mada nyingine jambo ambalo limewaongezea utaalamu na mbinu mpya kiutendaji hivyo kwenda kufanya kazi kwa kujiamini zaidi.
"Kwakweli Sekta ya mifugo inakwenda kupata mabadiliko makubwa kupitia elimu hii, maana tumejifunza kwa uhuru sana watoa mada wamekuwa wakitusikiliza na kutujibu kwa ufasaha maswali yetu, binafsi nimepanua upeo kwenye mambo ya mifugo kama ufugaji bora na wa kufuata kanuni za ufugaji wenye tija hivyo ninakwenda kuwapa wafugaji elimu hii, pia nimejifunza mambo mengi yanayohusu haki za mtumishi wa Umma" Alisema Agne
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.