Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndg. Musa J. Magufuli amewaomba watumishi wote walioshiriki katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano katika Halmashauri ya wilaya ya Chato mapema hii leo Disemba 04, 2023
Aidha katika kuhakikisha mafunzo hayo yanakuwa na tija kwa Ndg. Musa ameomba kila mtumishi kuhakikisha kila mshiriki anakuwa msikivu kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha kila ofisi zote za Serikali zinakuwa na taarifa sahii juu ya mahitaji na uwiano wa watumishi katika Idara na Sekisheni.
Katika hatua nyingine Ndg. Musa amesisitiza uwajibikaji na utoaji wa taarifa sahihi kwa kuweka majukumu yanayopimika katika utendaji wa kazi tofauti na kufanya hivyo amesema “ sisi kama watumishi wa umma tutakuwa hatujamsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Awamu ya Sita”
Katika hatua nyingine wakufunzi wa mafunzo hayo toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndg. Methew Nsolezi ambaye ni Afisa Utumishi na Ombeni Kasayo ambaye ni Mtakwimu wakitoa wafunzo hayo ya mfumo wa kufanya tathimini ya watumishi wametoa angalizo juu ya utoaji na uibuaji wa majukumu sahihi yanayoendana na kitengo au idara husika kwani kazi hizo ndo msingi katika kupata idadi na uwiano sahihi ya watumishi kwa kila Halmashauri na Taasisi ya Umma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Mandia H.Kihiyo ameishukuru Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuandaa mafunzo hayo kwani kupitia mafunzo haya ni matumaini makubwa sasa Halmashauri zote nchini zitakwenda kuondokana na uhaba au upungufu wa watumishi kwani mfumo huu unakwenda kujibu mahitaji sahihi kutokana na kazi za Idara au kitengo pasipo upendeleo wala kujuana.
Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani kumekuwa na malalamiko katika ugawaji wa watumishi na hivyo kupelekea baadhi ya maeneo kuonekana kuwa na watumishi wengi kuliko maeneo mengine hasa maeneo ya pembezoni.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.