Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Said Juma Nkumba, leo April 21, 2024 amefungua mashindano ya mpira wa miguu yaliyopewa jina la Muungano CUP ikiwa ni katika kuzisaka timu zitakazo fuzu kuingia fainali na kucheza siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 2024.
Mashindano hayo yamefanyika katika uwanja wa Mazaina wilayani hapa huku washiriki wakiwa ni timu ya kijiji cha Mkuyuni dhidi ya timu ya kijiji cha Rubambangwe na kuhudhuliwa na mamia ya wananchi wakiongozwa na Mhe. Mkuu wa wilaya, Katibu tawala (W), kamati ya ulinzi na Usalama (W) pamoja na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chato.
Katika Mtanange huo mkali, timu ya Mkuyuni imeibuka kidedea baada ya kuinyuka timu ya Rubambangwe magoli 04 kwa 01 huku wafungaji wakiwa ni ; Jezi na. 06 - Peter James goli 01 na Mkuyuni wakiwa ni jezi na.09 - Salehe Hamis Magoli 03 na Jezi na. 03 - Maneno Anthony goli 01
Mhe. Nkumba amewapongeza washiriki wote waliocheza leo kwa namna kila mmoja alivyoonesha ufundi wake uwanjani huku akiwataka waendelee na mazoezi zaidi kwa mechi zinazofuata ambapo amesisitiza kuwa mashindano hayo ni ishara ya kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hivyo kila mwananchi ashiriki kwa nafasi yake.
Kwa upande wake Afisa michezo wa halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg Abel Mataba Elias, ametoa ratiba ya ligi hiyo ya Muungano CUP kuwa 21/04/2024 wamecheza timu ya vijiji vya Mkuyuni na Rubambangwe, 22/04/2024 watacheza Muungano FC dhidi ya Chato Combine FC wakati 25/04/2024 ni fainali kati ya mshindi wa mchezo wa 01 na wa pili.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.