Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Chato, Ndg. Louis P. Bura leo Agosti 19, 2025 ametembelea na kukagua njia ya Mbio za Mwenge unaotegemewa kupokelewa wilayani humo tarehe 6 September 2025 ili kujionea maandalizi yanaendeleaje.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa wilaya ameridhishwa na hatua zilizofikiwa katika maandalizi, akisisitiza umuhimu wa sherehe hizo kama alama ya Umoja, Mshikamano na Maendeleo katika Taifa letu.
Aidha, amewapongeza Wakuu wa Idara mbalimbali kwa usimamizi mzuri wa Miradi ya Maendeleo inayofanyika wilayani humo, huku akisisitiza kuwa hayo ni matokeo ya kuwa ushirikiano kati ya Sekta za Umma na Binafsi katika kusimamia wa miradi hiyo, ambapo wameahidi kuendelea kutoa huduma bora na kuhakikisha maendeleo endelevu kwa wananchi wote wote na si kwa Miradi ya Mwenge bali Miradi yote inayotekelezwa ndani ya wilaya ya Chato.
Mwenge wa Uhuru, utapokelewa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nyakayondwa kata ya Bwanga ukitokea wilaya ya Bukombe na Utakesha Chato Mjini Viwanja vya Ma-zaina ikiwa na kauli mbiu isemayo; "Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa Amani na Utulivu"
Aidha Mwenge wa Uhuru utakapokuwa wilayani Chato utazindua na kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo na kuweka Mawe ya Msingi.maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea kwa kasi, huku wananchi wakihimizwa kushiriki kwa wingi katika Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwani ni Ishara ya uhuru na Maendeleo ya Taifa letu.
Wito umetolewa kwa wana chato wote kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Sherehe ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwani ni tukio muhimu linalo onyesha Umoja na Mshikamano, hivyo Kila mmoja anakaribishwa kushiriki na kuonyesha upendo kwa nchi yake katika tukio hili la kihistoria.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.