Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato Bi. Martha Mkupasi akizungumzana wananchi wa katika eneo la shule ya Msingi Katemi alipokuwa akizindua kampeni ya Upandaji Miti ikiwa ni moja ya shughuli za kijamii katika kuelekea katika kilele cha Sherehe za Uhuru ifikapo Disemba 9 mwaka huu.
Amesema pia tutapanda miti kwa ajili ya kupambana na Mabadiriko Tabia Nchi, ‘ndugu zangu wananchi wa maeneo haya niombe kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki katika zoezi hili la upandaji wa miti kwani kwa kufanya hivyo sote kwa pamoja tutakuwa tumeamua kupambana na athari zitokanazo na mabadiriko ya tabia nchi’
Ameongeza kwa kusema Chato hii siyo ya kukosa chakula au kuwa na upungufu wa chakula niombe kila mmoja atunze mazingira kwani ni sisi wenyewe ndio tunaoathirika baada ya kuharibu mazingira yetu.
Pia katika juma la kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Nchi yetu Mhe. Mkupasi amewaomba wananchi wote ndani na nje ya wilaya ya Chato kuendelea kujitokeza katika shughuli mbalimbali za kijamii kama ambavyo Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa sherehe ya safari hii tusheherekee katika maeneo yetu kwa kutafakari hatua tuliyofikia tangu kupata Uhuru, huku akielekeza fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya Maadhimisho ya sherehe za Uhuru Kitaifa kwenda kujenga Mabweni katika shule za watoto wenye Mahitaji maalumu.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Chato amewaomba wananchi wa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya Kilele cha Sherehe za Uhuru hapo tarehe 9 Disemba yatakayofanyika katika ukumbi wa Shule ya Skondari Jikomboe, pamoja na kuwaalika wananchi amesema siku hiyo kutakuwa na Mdahalo kuhusu Chimbuko la Uhuru wa Nchi yetu hivyo sote tufike kujifunza na kutoa maoni yetu.
Mhe. Diwani wa Kata ya Muungano Bw Charles Juma akitoa nenola shukrani amemwakikishia Mhe. Mkuu wa wilaya kuwa maelekezo na maagizo yote aliyoyatoa wao kama kata wanakwenda kukaa na Serikali ya kijiji kuhakikisha yote yanasimamiwa na kutekelezwa kikamilifu.
Nao wananchi waliofika katikauzinduzi wa Kampeni hiyo ya Upandaji Miti wamemshukuru Mhe. Mkuu wa wilaya na kumwahidi kuwa miti yote iliyopandwa wataitunza na kuilinda kwa ajili ya kizazi cha leo na kesho.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.