Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan ametoa mikopo yenye thamani ya Tsh.Million 475 kwa vikundi vya akina Mama Million 190 (4%) Walemavu Million 95 (2%) na Vijana Million 190 (4%) ambapo Vijana wamekabidhiwa pikipiki 39 leo Feb 17,2025. Katika Uwanja wa Stendi ya Zamani Chato.
Mgeni rasmi katika utoaji mkopo hiyo alikuwa Mbunge wa jimbo la Chato Dr Medard Kalemani na katika hotuba yake
Kwanza amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kwa mkopo huo ambao utakuwa chachu ya Maendeleo kwa wanachato.
Pia amewataka viongozi wanaosimamia mikopo kuhakikisha wanatoa mikopo hiyo kwa haki bila upendeleo wa aina yeyote.
Sambamba na hilo Dr Medard Kalemani amemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato ambulance mpya itakayotumika Kutoa huduma katika kituo cha afya Kachwamba.
Wakati huo huo amesisitiza kuwa miradi wa taa za barabarani ufanyiwe marekebisho kwa taa ambazo hazifanyikazi zitengenezwe ili zifanye kazi kama ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo amewataka wanavikundi wote wanaoomba mikopo kuhakikisha wanakidhi vigezo vinavyohitajika ili kuweza kupata mkopo na kuzingatia maelekezo wanayopewa na Maafisa Maendeleo ya jamii. Pia amewataka kujitayarisha kwa mkopo mwengine utakaotoka mwezi wa Nne.
Pia amewataka wanufaika wa mkopo kurejesha kwa wakati bila usumbufu ili mikopo hiyo inufaishe wanufaika wengine.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.