Zaidi ya shilingi milioni 431.2 zimetumika kwaajili ya kutekeleza mradi wa uchimbaji visima vitano kwenye vijiji vilivyokuwa na ukosefu mkubwa wa maji safi na salama kwenye Jimbo la Chato mkoani Geita.
Huo ni mpango mkakati wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo imetoa fedha kwaajili ya kuchimba visima 900 nchi zima ili kunusuru maisha ya wananchi wa vijijini ambao walikuwa hawajafikiwa kabisa na huduma za maji ya bomba.
Mkuu wa wilaya ya Chato,Louis Bura(katikati) akizungumza na wananchi wa Kibumba.
Meneja wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) wilayani Chato,Avitus Exavery, amesema hayo mbele ya mkuu wa wilaya hiyo ambaye alikuwa katika ukaguzi wa miradi ya mahi vijijini na kusikiliza kero mbalimbali.
vijiji vilivyo nufaika na mpango huo katika Jimbo la Chato kuwa ni Ludeba,Nampalahala, Nyantimba,Malebe na Kibumba.
Amesema miradi hiyo inakusudia kuwanufaisha wananchi zaidi ya 33,745 waliopo katika maeneo ya vijijini kwenye Jimbo hilo na kwamba hadi kufikia Mei 30,2025 upatikanaji wa maji kwenye vijiji hivyo utakuwa aslimia 60.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Kibumba,Clement Guri,mbali na kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa ya kuondoa adha kwa wananchi wa vijijini amesema huduma hiyo ni muhimu sana kwa wakazi wa eneo lake kutokana na vyanzo vingi vya maji kuchafuliwa na shughuli za uchimbaji madini.
Mkuu wa wilaya ya Chato,Louis Bura(wa kwanza kulia) akikagua chanzo cha maji katika mradi wa Kibumba,wa mwisho Kushoto ni Meneja wa Ruwasa,Avitus Exavery.
“Mradi huu kwetu ni mkombozi mkubwa kwa maana maji yaliyokuwa yakitumiwa na wananchi awali kwaajili ya kunywa,kunawa,kupikia,kuoga na matumizi mengine yalikuwa yakichafuliwa na shughuli za uchenjuaji Madini” amesema Guri.
Akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti jimboni humo,Mkuu wa wilaya ya Chato,Louis Peter Bura, amewataka wananchi kutambua uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo unaoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita kwa manufaa mapana ya Umma.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.