Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Chato ikiambatana na timu ya Menejimenti ya halmashauri mnamo Julai 22, 2025 ilifanya ziara ya kutembelea na kukagua njia na miraadi iliyopendekezwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru, yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 3.1 inayotekelezwa wilayani humo.
Ziara hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Louis Peter Bura ilianza ukaguzi wake katika eneo la Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yatakayofanyika shule ya msingi Nyakayondwa iliyopo kijiji cha Nyarututu kata ya Bwanga.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na ziara hiyo ni ujenzi wa zahati ya kijiji cha Nyarututu kata ya Bwanga (92,410,714.29) chanzo cha fedha ni TASAF, mradi wa usambazaji maji kijijini (RUWASA) uliopo kijiji na kata ya Minkoto (263,413,920.16) chanzo cha fedha ufadhili wa benki ya Dunia (P4R) zaidi ya wananchi 5724 wananufaika na mradi, mradi wa uzaliahaji wa vifaranga na ufugaji samaki-Rumasa (7.000,000/=) chanzo cha fedha mikopo ya vijana 10% mapato ya ndani ya halmashauri, Boksi karavati barabara ya Mranda - Imwelu kata ya Buseresere (399,999,928.20) chanzo cha fedha ni ufadhili wa Benki ya Dunia mradi umekamilika na unatumika.
Pia ziara ilikagua ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya msingi Nyabilezi kata ya Bukome (50,000,000/=) fedha za mapato ya ndani ujenzi wa boma unaendelea, ujenzi wa shule ya Sekondari mpya Kitela kata ya Chato (500,000,000/=) kutoka Serikali kuu, shule imekamilika na inatumika, mradi wa uzalishaji samaki uliopo ndani ya mradi wa ujenzi wa chuo cha uvuvi kinachojengwa kijiji cha Rubambangwe kata ya Muungano (1,540,677,372/=) fedha kutoka Serikali kuu ujenzi upo 75%, pamoja na ukamilishaji wa Bwalo la chakula sambamba na jiko ambalo litafungwa mfumo wa nishati safi ya kupikia Shule ya ufundi stadi Chato( Chato Technical School) (262,754,041/=) fedha kutoka Serikali kuu.
Timu hiyo iliendelea na ukaguzi kwa kutembelea chanzo cha maji na upandaji miti katika kijiji cha Minkoto shamba la miti Silayo, Shule za Sekondari Buseresere na Buzirayombo pamoja na Kukagua Klabu ya kupambana na kuzuia Rushwa na madawa ya Kulevya Shule ya Sekondari Mkungo kata ya Bukome.
Kwa upande wake mratibu wa Mwenge wa Uhuru wilayani Chato Ndg Halfan Mbonde alieleza namna maandalizi yalivyofikia hatua nzuri kwa kila kamati kutimiza majukumu yao na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Wilaya ya Chato inatarajia kuupokea Mwenge wa uhuru mnamo tarehe 06 Septemba 2025 ukitokea wilayani Bukombe, ambapo utakagua miradi na mbalimbali na baadaye kukesha katika uwanja wa Maz-aina uliopo kata ya Chato. Kauli ikiwa ni “JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU”
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.