Ikiwa umebaki mwezi mmoja tu kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024 Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa imevitaka vyama vya siasa Wilaya ya Chato kuzingatia Kanuni na Sheria za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinazotolewa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.
Akizungumza katika kikao cha ndani mapema hii leo Oktoba 23, 2024 Ofisa wa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Ndg. Dinna Mcharo, amesema; " viongozi wa Vyama vya Siasa Chato nendeni mkatekeleze majukumu yenu kwa kuzingatia Kanuni pamoja Sheria ambazo mmepewa kama msaafu katika kufanya shuhguli na hasa katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa"
Aidha Bi. Dinna amevitaka Vyama vya Siasa kwa kipindi hiki cha maandalizi ya kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuheshimu sheria zinazosimamia uchaguzi pamoja na kuzingatia kanuni za maadili ya vyama vya siasa na pamoja na kanuni zinazoratibu mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa.
“Ni wajibu wa chama cha siasa kulaani, kuepuka na kuchukua hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria ili kuzuia au kuepusha vitendo vya vurugu, kutumia nguvu, matumizi ya lugha za matusi, uvunjifu wa amani na ukandamizaji wa aina yoyote”
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.