Mkuu wa wilaya ya Chato mkoani Geita, Louis Bura,amewataka wananchi kudumisha amani, mshikamano na umoja wa kitaifa hasa kuelekea kwenye Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani nchini.
Aidha amesema Msingi wowote wa maendeleo lazima utokane na wananchi wenyewe na kwamba mahali popote ambapo pana umoja hutawaliwa na amani.
Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Chato kwenye kata ya Nyamirembe katika maadhimisho ya kilele cha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Bura amesema ni muhimu jamii kutambua mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia muungano huo badala ya kukaa vijiweni na kukosoa mapungufu machache yanayojitokeza.
"Wakati nchi hizo zinaungana mwaka 1964 zilikuwa maskini sana, lakini kutokana na maono mema ya waasisi wetu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume,nchi zetu zilifanikiwa kupiga hatua kubwa za kimaendeleo na hadi sasa viongozi wanaendelea kusimamia maono hayo,"
"Ukiona vya elea ujue vimeundwa,wapo wazee wetu waliopigania uhuru wa nchi hizi mbili kwa jasho na damu na hatimaye kufanikiwa kuziunganisha,hivyo niwasihi sana ndugu zangu tuendelee kuulinda muungano wetu kwa maslahi mapana ya taifa letu" amesema Bura.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Geriad Mgoba, amesema pamoja na mambo mengine halmashauri yake imefanikiwa kupanda miti 3,500 katika kuadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kulinda Mazingira.
Miti hiyo imetokana na ushirikiano mwema wa halmashauri ya wilaya hiyo pamoja na Wakala wa huduma za misitu (TFS) Chato ambao kwa pamoja wanakusudia kulinda,kudumisha na kuhifadhi uoto wa asili kwa manufaa ya watu, wanyama na viumbe hai wengine.
Mkakati huo unaungwa mkono na nukuu ya Mwanafalsafa Warren Buffet aliyesema "Anaekaa kivulini leo ni kwa sababu kuna aliyepanda mti muda mrefu uliopita,"
Hali Kadhalika, Chinese Proverb aliwahi kusema “Muda mzuri wa kupanda mti ni miaka 20 iliyopita, Lakini muda mwingine mzuri wa pili ni sasa.”
Hatua hiyo inaonyesha wazi kuwa jukumu la kuhifadhi misitu,kulinda vyanzo vya maji na Usafi wa Mazingira ni hazina kubwa kwa maisha
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.