Katika kuadhimisha sherehe ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wilaya ya Chato jana April 22, 2024 imeshiriki kufanya usafi katika mazingira ya kituo cha afya Bwina zoezi lililoenda sambamba na kupanda miti maeneo hayo ikiwa ni ishara ya kuuenzi Muungano huu.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Said Nkumba ambaye alisisitiza suala la kuendelea kuulinda na kuudumisha Muungano wetu ili tuendelee kuwa na amani na utulivu lakini pia kuilinda Tunu hii adhimu tuliyoachiwa na waasisi wetu huku akiitaja kauli mbiu ya Muungano 2024 kuwa ni " Tumeshikamana, tumeimarika kwa maendeleo ya Taifa letu"
Sambamba na hayo pia alitembelea na kukagua kituo hicho namna kinavyofanya kazi kwa kuzungumza na wagonjwa jinsi wanavyopata huduma nao walikiri kuhudumiwa vizuri huku wakiwapongeza wauguzi jinsi wanavyowajali, ndipo alimuhoji mganga mfawidhi juu ya madawa na vifaa tiba ambaye alikiri hakuna tatizo hilo kwasasa hivyo wanatoa huduma kwa wagonjwa bila kikwazo chochote.
Aidha Nkumba aliwawapongeza wananchi waliojitokeza katika kazi hiyo na watumishi wa halmashauri kwa namna wanavyoonesha ushirikiano katika shughuli za maendeleo na pongezi nyingi kwa wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa kuleta miti 300 ya matunda na kivuli iliyopandwa kituoni hapo na mingine itapandwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Chato, ambapo aliwataka wote waliopewa miti hiyo kuitunza vizuri.
Diwani wa kata ya Bwina Mhe. Reginald Gervas Mbani ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kazi kubwa na nzuri inayoifanya ya kuboresha miundo mbinu kuanzia kwenye elimu, maji, barabaraba pamoja na Afya ukiachana na kuimarisha miundo mbinu yake pia imemaliza tatizo la upungufu wa dawa na vifaa tiba kwa ujumla, wananchi wanapata huduma vizuri
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.