Serikali Wilayani Chato imeonya tabia ya baadhi ya wanafunzi wa kike kuwaficha wanaume wanaowapa ujauzito pindi wanapofikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kiwilaya kata ya Nyamirembe.
Mkuu wa Wilaya amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanafunzi wa kike kuficha taarifa za waliowapa mimba na kusema kuwa kuanzia sasa serikali itakuwa inawachukulia hatua wenyewe kwani tatizo la mimba mashuleni limekithiri sana.
“naomba niwatangazie kuanzia sasa wanafunzi wa kike ukipata ujauzito na ukamficha aliyekupa ujauzito au ukimsaidia kutoroka tunakushitaki wewe mwenyewe” alisisitiza Mkuu wa Wilaya
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Chato amewaasa wanawake wote kutoa taarifa juu ya unyanyasaji na unyanyapaa wanaofanyiwa wanawake majumbani na mahali pa kazi. Amewataka wanawake kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola hususan TAKUKURU.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2019 ilikuwa “Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu”
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.