Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt Zainab Chaula akikagua moja ya jengo la zahanati ya Katete kata ya Bwongera
Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt Zainab Chaula akiangalia miundombinu katika zahanati ya Katete kata ya Bwongera
Mzee Rashid Milambo (wa katikati)mkazi wa Mbuye kata ya Bwina ambaye ni mmoja ya wananchi wenye maeneo waliopisha ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Bwina akiwa na Naibu katibu Mkuu ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. zainabu Chaula
Serikali kupitia wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na watoto imeendelea kuboresha sekta ya afya Wilayani Chato kwa kuanza kukarabati zahanati na kuzipandisha hadhi kuwa vituo vya afya sambamba na kujenga vituo vipya viwili Wilayani hapa.
Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt. Zainabu Chaula amefanya ziara na kuvikagua zahanati ambazo zinatakiwa kufanyiwa ukarabati pamoja na maeneo ambayo Halmashauri imependekezwa kujengwa vituo vya afya.
“Tuna changamoto ya miundombinu ya sekta ya afya, kwani iliyopo haitoshi na si ya kuridhisha na nyingine ni za zamani sana, kwa hiyo tunataka kupunguza changamoto kwa kuboresha vituo hivi hivi viliyopo” alisema Dkt. Chaula.
Amesema kutokana na Wilaya ya Chato kuwa na vituo vya afya vitatu tu vinavyofanya kazi ukilinganisha na idadi ya watu 419,000 waliopo kuna ulazima wa kuboresha zahanati zingine na kuzipandisha ili viwe vituo vya afya.
Dkt. Chaula amesema pia kutokana na changamoto ya raslimali watu ni vyema Halmashari zikajielekeza zaidi kuboresha zahanati na vituo vya afya vilivyopo badala ya kuanzisha maeneo mapya ya ujenzi.
Naibu katibu Mkuu amepongeza pia jitihada zinazofanywa na Halamashauri za ujenzi wa zahanati katika kila kijiji na vituo vya afya kila kata ambapo amesema wananchi waelimishwe na kuhamasika kushiriki kazi ambazo jamii inahusika katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya sekta ya afya.
Zahanati zitakazoboreshwa na kupandishwa hadhi ya kuwa vituo vya afya ni ya kata ya Ilemela, Katete kata ya Bwongera na vituo vya afya vitakavyojengwa ni pamoja na vya kata ya Buseresere na Bwina ambapo Naibu katibu Mkuu ametembelea maeneo yote hayo pamoja na wataalamu kutoka wizara ya Afya na Fedha.
Kukamilika kwa ukarabati wa vituo hiyo utasaidia wananchi wapatao laki moja wa kata hizo kufuata huduma za afya katika hospitali ya Wilaya ya Chato umbali wa kilometa 80 kutoka kata ya Busereser na 50 kutoka Katete kata ya Bwongera.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.