Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Said Nkumba, jana Mei 15, 2024 akiwa mgeni rasmi alifungua kikao cha Jumuiya ya wafanya biashara wa wilaya hiyo kilichoketi katika ukumbi wa Mshikamano SACOS uliopo Chato mjini ambapo aliwataka T.R.A kuendelea kutoa elimu ya kodi na kufuatilia matumizi ya EFD mashine ili kumsaidia mfanya biashara kutokadiriwa malipo ya kodi na pia awe na utashi na hiari ya kulipa bila kufuatiliwa.
Kikao hicho kiliandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kuratibiwa na Afisa Biashara wilaya huku washiriki wake wakiwa ni wafanya biashara wote wakubwa na wadogo, wawezeshaji ni NSSF, GGML, BUCREEF GOLD MINE LTD, SIDO, Ofisi ya Afisa Madini Mkoa wa Geita (RMO), Bomba la mafuta, TRA pamoja na taasisi za fedha kama NMB, CRDB na Azania Benki.
"Nawapongeza kwa mahudhurio mazuri mmeitikia wito, kwani kikao hiki kina faida kubwa sana kwenu, lengo ni kuwajengea uwezo wafanya biashara wetu pamoja na kuwakutanisha na fursa mbalimbali, Serikali inatambua umuhimu wa kundi lenu katika kukuza uchumi, kwakuliona hilo ndio maana tumekutana hapa. Nawaelekeza TRA elimu ya tozo, kodi, na ushuru iwe endelevu ili nanyi wafanya biashara kulipa kodi hizo iwe ni utashi na hiari yako kwa kuepuka usumbufu lakini pia ni uzalendo". Alisema Mhe. Nkumba
Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanya biashara wilaya ya Chato Ndg. Daud Mbeshi aliwapongeza na kuwashukuru Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi kwa kuandaa kongamano hilo lililowakutanisha wafanya biashara wote wa wilaya na wawezeshaji walio wajengea uwezo kiasi kwamba amekiri kuelewa vizuri namna ya kuchangamkia fursa na kuboresha uendeshaji wa biashara zao.
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo alikifafanulia kikao hususani wageni kuwa wilaya hii ina jumla ya vijiji 115, kata 23, tarafa 5 na wakazi 584,963, fursa zilizopo ni miundo mbinu ya barabara mizuri, hali ya hewa nzuri, ziwa viktoria, hospitali ya kanda na ya wilaya, miradi mingi ya Serikali na ardhi yenye rutuba inayofaa kilimo msimu huu tunatarajia kuvuna mpunga tani 40,000
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.