Katibu Tawala wilaya ya Chato Mkoani Geita Ndg Thomas Dimme kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Louis Peter Bura ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati, ameongoza kikao cha kamati ya lishe wilaya cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa tathmini ya mkataba wa afua za lishe katika kipindi cha robo ya kwanza mwaka wa fedha 2024/2025.
Kikao hicho kimefanyika jana Disemba 06, 2024 katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa wilaya ambapo wajumbe waliohudhuria ni kutoka idara na vitengo mbalimbali wakiwemo idara ya afya, Kilimo ufugaji na uvuvi, Ustawi wa jamii, Maendeleo ya jamii, elimu Sekondari, elimu Msingi pamoja na watendaji wa Kata.
Akiwasilisha taarifa hiyo, Afisa lishe wilaya ya Chato Ndg Izack Malongo amesema kuwa katika kipindi cha robo ya kwanza Julai - Septemba 2024/2025 shule 221zimetekeleza agizo la kutoa chakula shuleni huku wakizingatia suala la lishe bora kati ya shule 222 zilizopo ikiwa ni za Msingi na Sekondari.
Malongo amesema kuwa katika kipindi hicho wametembelea kata kumi na moja kwa kupita vijijini kukutana na uongozi wa maeneo hayo kufanya mikutano yenye kutoa elimu juu ya lishe bora pamoja na umuhimu wa kutoa chakula kwa wanafunzi wawapo shuleni huku akibainisha changamoto ya wazazi/walezi kuwapeleka watoto wenye utapiamlo kwenye tiba asili badala ya hospital ambapo pia elimu ilitolewa.
Naye Mganga Mfawidhi wa halmashauri hiyo Dkt. Aristides Raphael amesema timu ya wataalam wa afya na lishe wanaendelea kutoa elimu katika jamii kuanzia ngazi ya kata na vijiji kwenda kukutana na uongozi wa maeneo hayo pamoja na wananchi kuwapa elimu zaidi ya lishe bora ili kupambana na utapiamlo na udumavu lakini pia kuwajengea uwezo wa kutambua umuhimu wa lishe lengo ni kupata jamii yenye afya njema.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Ndg. Mandia Kihiyo amesema lishe imepewa kipaombele katika wilaya,ili kuimarisha afya ya kila mmoja huku akikazia umuhimu wa kuwapa chakula wanafunzi wawapo shuleni ikiwa ni nguzo ya kuinua taaluma lakini pia hukomesha utoro hatimaye kuongeza ufaulu,huku akishauri kamati kuhimiza jamii kula vyakula
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.