Jumla ya vikundi 21 vya vijana, Wanawake na walemavu kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato vimenufaika na mikopo inayotolewa na Halmashauri kupitia fedha za mapato ya ndani.
akikabidhi mikopo hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 39 Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri ameviasa vikundi hvyo kutumia kwa uangalifu fedha hizo ili badae vikopeshwe tena fedha zaizdi ya hizo walizokopeshwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliurd Mwaiteleke amesema fedha izo zinazotolewa na Halmashauri ni fedha za mapato ya ndani na ukusanyaji wa mapato ukienda vizuri kwa mwaka huu wa fedha fedha ambazo zitatolewa zitakuwa ni milioni 220 ambapo hadi sasa jumla ya shilingi milioni 84 zimekwisha tolewa kwa walengwa
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.