Diwani wa kata ya Kasenga mhe. Damian Zilaliye amesema iwapo viongozi kuanzia ngazi za vitongoji hadi Wilaya wakishirikiana vizuri na wananchi wao ujenzi wa miundombinu ya sekta ya afya itakamilika mapema sana.
Mhe. Zilaliye amesema hayo wakati akipokea mifuko 20 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Chato aliyoahidi hivi karibuni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kata ya Kasenga.
"Hawa wananchi wengi unaowaona hapa ni kwa sababu wameukubali huu mradi na wanaendelea kuchangia kila siku ili kituo hiki cha afya kikamilike mapema" alisema mhe. Diwani.
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Chato ndugu Elias Makory aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chato katika ziara ya kukagua na kukabidhi mifuko ya saruji iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya amesema ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Kasenga ni mapinduzi makubwa sana kwani utarahisisha upatikanaji huduma za tiba karibu na wananchi.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Ichwankima mhe. Denice Joseph amesema ziara za viongozi kwenye maeneo mbalimbali zinahamasisha sana wananchi kushiriki katika kazi za ujenzi na utoaji wa michango.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chato Dkt. Athanas Ng'ambakubi amesema ushiriki wa wananchi katika ujenzi wa zahanati na vituo vya afya ni matokeo ya ushirikishwaji wa wananchi katika kujiletea maendeo ambapo amesema kama ushiriki huu wa wananchi utaendelea kwa kasi ujenzi wa Miundombinu ya sekta ya afya utakamilika mapema sana.
Jumla ya mifuko 26 yenye thamani ya shilingi 520,000 imekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vya kata ya Kasenga na Ichwankima.
Wilaya ya Chato imeunda kamati ya uhamasihaji na ufuatiliaji wa ujenzi wa Miundombinu ya sekta za afya na elimu yenye lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika kwenye kazi za mikono na michango pamoja na usimamizi wa ubora wa Miundombinu hiyo.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.