Mkuu wa wilaya ya Chato Mh. Deusdedith J. Katwale amewasisitiza viongozi na waajiri wote kuipa kipaombele elimu ya dini hususani shuleni kuwepo na vipindi vya dini ikiwa ni mikakati ya kurejesha maadili Kwa watoto na jamii Kwa ujumla.
"Kuanzia leo Kwa maana ya kujitambulisha na kujipambanua kama Wilaya ya Chato, ikiwa ni mikakati ya kurejesha maadili elimu ya dini ipewe kipaombele na itakuwa kipindi Cha kwanza Kila siku ya jumatatu, Mkurugenzi upo hapa na Afisa elimu upo nendeni mkawaagize waratibu elimu kata kulisimamia Hilo." Amesema Katwale.
Mh. Katwale ameyasema hayo wakati akihutubia kwenye mkutano wa kufunga juma la maombi mnamo 27 Julai 2023 ikiwa maombi hayo yalianza 21 Julai 2023 ambapo aliwataka viongozi na watoa huduma Kwa jamii kutoa huduma nzuri na stahiki Kwa jamii wanayoihudimia Ili kudumisha amani, upendo na Furaha Kwa jamnii.
Hata hivyo Mh Katwale aliongeza kuwa amedhamiria kuibadilisha chato na kuwa ya kijani Kwa Kila kaya kupanda miti hususani miti ya matunda itakayowasaidia kiafya lakini pia kiuchumi jambo ambalo litaleta muonekano wa tofauti hata Kwa wageni watakao fika Chato.
Akizungumza Kwa niaba ya viongozi wa madhehebu ya kikristo katika Wilaya ya Chato Mchungaji wa kanisa la Anglikana Zacharia Samson amemshukuru Mh. Mkuu wa wilaya Mhandisi Katwale kuwa na maono ya mbali kupata wazo la kuwakutanisha viongozi wa dini ya kikristo na kiislam kufanya maombi ya pamoja ikiwa ni kuombea Wilaya iwe yenye amani na upendo.
Mchungaji Samsoni wongeza kuwa penye amani pia mafanikio yanapatikana, hivyo Nia njema ya mkuu wa Wilaya ya kuiweka Chato mikononi mwa Mungu ni dhamira ya kuhakikisha Wilaya inakuwa na mafanikio makubwa katika Kila sekta Hali ambayo itainua uchumi wa mwananchi Mmoja Mmoja hatimaye Wilaya na Taifa Kwa ujumla.
Akitoa neno Shehe mkuu wa wilaya ndugu Abdurahman Ismail amesiaitiza juu ya kuilinda amani kuwa si suala la viongozi wa dini pekee bali ni suala la Kila mwananchi kuhakikisha anailinda amani Kwa juhudi zote, endapo amani ikianzia ngazi ya familia italeta manufaa hata ngazi ya Wilaya na Taifa Kwa ujumla.
Shehe Ismail amewataka wananchi wa Chato kuendelea kuungakono juhudi za Mkuu wa wilaya Mh Katwale Ili kuinua uchumi wa kaya na Taifa, ameongeza kuwa inatupasa kumtanguliza Mungu mbele Kwa Kila jambo.
Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Chato ndugu Mandia Kihiyo amekiri kufurahishwa na wazo la mkuu wa wilaya kuwatumia viongozi wa dini na madhehebu yote kuiombea Wilaya, pia ameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha na kusimamia utekelezaji wa yote aliyomuagiza hususani elimu ya dini shuleni.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.