Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na wadau (USAID)yenye Nia ya kuboresha afya na lishe katika jamii yamefunguliwa na mkurugenzi mtendaji Ndg Mandia Kihiyo Agosti 16 2023 katika ukumbi wa halmashauri ya Chato, walengwa wakiwa ni waheshimiwa madiwani, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji, maafisa Ugani, wenyeviti wa vijiji pamoja na wenyeviti wa vitongoji Kwa maeneo ya kata 7 na vijiji 10 vilivyoteuliwa vigezo vikiwa ni kuwa mbali na huduma ya afya.
Katika mafunzo hayo, Afisa lishe Wilaya Ndg Renatus Kimba amewafundisha viongozi namna ya kupangilia Milo Kwa kutumia Vyakula vinavyopatikana katika mazingira yao kama vile nafaka, vyakuka vya mizizi na ndizi mbichi, Vyakula vya asili ya wanyama na jamii ya mikunde, mbogamboga, mafuta na matunda.
"Viongozi wenzangu elimu hii ya afya na lishe ikawe ni ajenda ya Kila kikao na mikutano katika vijiji vyenu na kata (WDC) ,
Nawasisitiza watendaji wa vijiji mkateue mratibu wa siku ya lishe na afya kutoka kwenye kamati ya ustawi wa jamii ya Kijiji na muhakikishe sherehe ya siku ya lishe na Afya inafanyika mara nne Kwa mwaka "Alisema Kimba"
Aidha, Mheshimiwa Salama Mgasa diwani wa kata ya Buziku, ameipongeza serikali kuwapatia elimu hiyo na kukiri kuwa itawasaidia kupunguza au kutokomeza kabisa udumavu, kwani jamii licha ya kuwa na Vyakula vyote vyenye virutubisho lakini wanakosa elimu ya kuvipangilia Ili vilete manufaa kiafya.
Hata hivyo Mheshimiwa Mgasa alikazia suala la vikao na mikutano katika maeneo yao Ili kuwafikishia wananchi elimu hii adhimu itakayokuwa ni tiba katika harakati za kutokomeza udumavu.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.