Wilaya ya Chato imefanya kikao cha Baraza la Biashara la Robo ya tatu kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 lililofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita mnamo tarehe 17 Mei, 2024 ambapo Wafanyabiashara wamepigwa msasa wa kuwapatia elimu juu ya upatikanaji wa vitambulisho vya ujasiliamali pamoja na ulipaji wa tozo, ushuru na kodi.
Zoezi hilo limeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Wilaya, ambaye ni Mkuu wa wilaya Mhe. Said J. Nkumba likiwa na wajumbe 40 ambao kati yao 20 ni toka Sekta za Umma pamoja na 20 toka Sekta binafsi ambao ni wawakilishi wa wafanyabiashara waliochaguliwa toka katika makundi ya Wafanyabiashara wenye viwanda, Wakulima na Wafugaji ili kuwawakilisha wenzao.
Aidha Mhe. Nkumba ametumia kikao hicho kuwaasa wafanyabiashara kujijengea tabia ya kulipa ushuru na kodi kwa wakati bila kulimbikiza ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza kati yake na Serikali pindi atakapo kwama kuitoa kwa kuelemewa na kuwaelekeza wanaoshughulikia suala la ukusanyaji kodi kuwafikia kwa muda waliopangiana kuwapunguzia adha hiyo.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.