Waheshimiwa Madiwani katika Halmashauri ya Chato katika Baraza lilofanyika tarehe 16 Mwezi Februari 2023 katika ukumbi wa Halmashauri wametoa hisia kali juu ya mwenendo wa ukusanayaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri hiyo na kudai kuanzia sasa watakula sahani moja na mtumishi yeyote atakaye onyesha kukwamisha au kuhujumu juhudi za ukusanyaji wa mapato hayo ndani ya Halmashauri.
Wakichangia Wahe. Madiwani katika mkutano huo wa Baraza la Madiwani robo ya pili katika kupitia taarifa za Kata (WDC) pamoja na Taarifa za k
Kamati za Kudumu za Halmashauri wamesisitiza suala la mapato kila mmoja kuanzia watendaji wa Kata, vijiji na watumishi wote kuona jambo la mapato kama uti wa mgongo katika Halmashuri kwani bila mapato halmashauri haiwezi kujiendesha kwani kila kitu kinahitaji fedha mfano posho za madiwani, stahiki mbalimbali za watumishi na mambo mengine ya kiutendaji pamoja na uendeshaji wa Halmashauri kama mafuta ya magari.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Christian Manunga amewaomba Wahe. Madwani kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anakwenda kusimamia ukusanyaji wa mapato katika eneo lake.
Mhe. Manunga ameongeza kwa kusema kuwa, "Wahe. Madiwani wenzangu mpaka sasa Halmashauri yetu imekusanya shilingi 851,351,633.82 sawa na asilimia 39.60 ambapo tulitakiwa kuwa tumekusanya shilingi 1,075,000,000.00 sawa na asilimia 50 ya bajeti katika Mapato halisi ya ndani"
Pia Mhe. Manunga amekemea tabia ya baadhi ya watumishi kuwa na vikundi vya ujenzi ambavyo vimekuwa vikifanya kazi mbalimbali katika Halmashauri na hivyo makundi mengine yanayotoka kwa wananchi kukosa kazi na hivyo kupelekea malalamiko mengi hasa ya baadhi ya vikundi kuonekana kila kazi ya ujenzi vinafanya vyao na vingine kuonekana havina nafasi amemaliza kwa kusema acheni tabia hiyo mara moja.
Kwa upande wa Mhe. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Ndg. Jangole amewaomba watumishi kufanya kazi kwa uadilifu, ubunifu na uaminifu mkubwa ili sote kwa pamoja tuweze kuwaleta maendeleo wananchi wa Chato.
Mbunge wa Jimbo la Chato Mhe. Medard Kaleman kwa upande wake amewataka watumishi wote pamoja na wahe. Madiwani sote kwa umoja wetu ninaomba sana twendeni tukafanye kazi kama timu, hapa tulipofikia si mahala pa kulaumiana bali nikujisahihisha na kusonga mbele ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea.
Pia Mhe. Kaleman amemshukuru Mhe. Rais kwa jinsi ambavyo Serikali yake imekuwa na inaendela kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri yetu akitaja baadhi ya maeneo ambayo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetoa pikipiki 44 kwa ajili ya maafisa Ugani na pikipiki 7 kwa ajili ya watendaji wa kata lengo ikiwa ni kuboresha utendaji kazi katika maeneo yetu ya kiutendaji.
Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Deusdedith Katwale ameomba watumishi kuzigatia ushauri uliotolewa ndani ya kikao na kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ameomba kila mmoja akasimamie kile tulichokubaliana na ikitokea mtu ametukwamisha basi tumuondoe tubake na wale watakaotuvusha ikiwa ni pamoja kuhakikisha Halmashauri ije na mipango yenye tija ili Halmashauri hii itoke kwenye hii aibu ya kuonekana ipo chini katika ukusanayaji inaondoka na kuwa historia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Mandia Kihiyo ameahidi kutoa ushirikiano kwa kila diwani katika kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanapatikana na kukusanywa kikamilifu hukua akiahidi kutomfumbia macho mtumishi yeyote ambaye ataonekana anakwamisha au kuzuia zoezi la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwani kufanya hivyo ni kosa na hujuma kwa Halmashuri yetu.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.