Baadhi ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF III) wamejikita katika miradi ya ufugaji kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato cha kaya.
Wakiongea na timu ya wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya iliyowatembelea ikiongozwa na Mratibu wa TASAF bwana Alex Mang’ara baadhi ya wanufaika hao wamesema wameamu kuanzisha ufugaji wa mifugo mbalimbali ili kuongeza kipato cha kaya.
Wanufaika hao kutoka katika kijiji cha Nyambiti Wilayani hapa wamesema ufugaji ndio njia pekee itakayowanusuru na janga la umasikini.
“Nilipopata tu fedha za kwanza za mgao wa TASAF, nilitunza nikanunua Mbuzi wawili… hadi sasa nina mbuzi 19” alisema Bi. Lega Amos ambaye ni mmoja ya wanufaika wa mpango wa TASAF ambaye amesema matarajio yake ni kuuza Mbuzi hao ili ajenge nyumba bora na ya kisasa kufikia mwezi Juni 2018.
Naye Bi. Kabla Peter amesema kupitia ufugaji wa Mbuzi na Ng’ombe anaowafuga kutokana na fedha za TASAF anao mpango wa kununua shamba kwa ajili ya kuendesha shughuli za kilimo.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango huo bwana ;azaro Kajoro amesema kupitia fedha za hizo kumemwezesha kujenga nyumba nzuri ambayo iko katika hatua za ukamilishaji. Bwana Kajoro ameupongeza Mpango wa TASAF III kwani amesema kwake yeye umekuwa mkombozi wa maisha yake.
Bw. Mang’ara amewashauri wanufaika hao kutumia vyema fedha wanazo pata hasa kwa kuanzisha miradi ili badae waweze kuboresha makazi yao na kipato cha kaya.
Halamshauri ya Wilaya ya Chato inazo kaya 7,706 ambazo zinanufaika na Mpango wa TASAF awamu ya tatu ambapo kijiji cha Nyambiti kina jumla ya wanufaika 136.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.