WAZIRI JAFO AFURAHISHWA NA USIMAMIZI WA MAJENGO YA EP4R
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato kwa kusimamia vyema ujenzi wa miundombinu ya elimu hususan ile ya lipa kulingana na Matokeo (EP4R) iliyojengwa shule ya sekondari ya Magufuli iliyopo kata ya Bwanga.
Waziri Jafo amefurahishwa na uimara wa majengo hayo mara baada ya kufanya ziara na kukagua miradi ya EP4R ikiwemo Bwalo, Mabweni, madarasa na Matundu ya vyoo yaliyojengwa kwa fedha za mradi huo mwaka 2016/2017 ambapo ujenzi wote uligharimu kiasi cha shilinngi milioni 570,500,000.
Waziri Jafo pia ameupongeza uongozi wa shule hiyo ya Magufuli kwa kufanya vizuri katika matokezo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka 2017 ambapo shule hiyo ilishika nafasi pili kikanda, ya pili kimkoa na 22 kitaifa na kufanikiwa kuwamiongoni mwa shule 25 bora kitaifa. “Mimi naomba niwapongeze ninyi vijana wa Magufuli, kwa sababu kila ninaposoma kwenye mitandao shule yenu inafanya vizuri sana Tanzania” alisema Waziri Jafo.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Chato kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa Miundombinu mbalimbali katika kituo cha afya Bwanga ifikapo tarehe 12 Juni 2018.
Waziri Jafo amesema Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya nchi nzima lakini hadi mwezi Mei 2018 Wilaya ya Chato ilikuwa bado haijakamilisha ujenzi huo wa miundombinu hiyo kitu ambacho ni kinyume na maagizo ya serikali.
Ujenzi huo ambao utagharimu shilingi Milioni 500 kwa kutumia vibarua, umelenga kujenga miundombinu mipya na kukarabati majengo yaliyopo ambao kwa sasa kuna wodi wazazi moja na watoto, Maabara, nyumba mbili za watumishi, chumba cha maiti, chumba cha kufulia na Chumba cha dawa vinaendelea kujengwa.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.