Katika kuhakikisha Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya katika Halmashauri ya Chato vinatoa huduma bora, Shirika lisilol la Kiserikali (The Eleanor Foundation) limetoa msaada wa Magodoro 10 yenye thamani ya shilingi 1,200,000 ikiwa ni katika jitihada za kuhakikisha akina mama na watoto wanapata mazingira mazuri wakati wanapokwenda hospitalini hapo kupatiwa matibabu.
Akikabidhi msaada huo wa Magodoro Ndg. Sospeter Rwegoshora ambaye ni mjumbe wa bodi katika Shirika la Eleanor Foundation kwa niaba ya Shirika hilo ameiomba jamii kuonyesha mchango wake hasa katika maeneo wanayoomba kusaidiwa ili hata wao wanapokuwa wanapitia ni maeneo gani watoe msaada basi waanze na wale walioonyesha nia na utayari wa kupokea mradi au msaada ameongeza kwa kusema " unapoomba kusaidiwa anza wewe mwenyewe wengine wakikuona watakushika mkono pia kumbukeni mkono usiotoa na kupokea hakuna"
Aidha kwa nyakati nyingine Meneja Mradi shirika la Aleanor Foundation toka
Chato na Biharamulo Ndg. Godfrey Gahanga amewashukuru viongozi wote wa Chama na Serikali kwa namna ambavyo wamekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha Kituo cha Afya Mganza kinakuwa na mazingira mazuri ya kutolea huduma kwa wagonjwa.
Ndg. Gahanga ameongeza kwa kusema, katika kituo hiki cha Mganza huu sio msaada wetu wa kwanza mahala hapa tumekwisha saidia katika kuhakikisha kituo hiki kinapata maji safi na salama wakati wote na hiyo huduma teyari inafanya kazi pia huduma ya Solar kuhakikisha maeneo yote mhimu yanakuwa na umeme na mwanga wa uhakika mda wote mfano chumba cha kuhifadhia Damu, Maabara, Chumba cha upasuaji na wodi ya wazazi japo nia yetu ni kuhakikisha kituo chote kinakuwa kimeunganisha na mfumo wa umeme wa Sola.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Mganza amewashukuru sana Shirika la Eleanor Foundation kwa kusema "hakika sisi kama kituo hatuna cha kuwalipa ila kamwe hatutakuja kuwasahau kwani mmefanya mambo makubwa sana pengine bila ninyi tungechelewa sana kuwa na mazingira haya mazuri kwa ajili ya kutolea huduma kwa wagonjwa"
Akihitimisha hafla hiyo ya mapokezi ya msaada huo wa Magodoro Mganga Mkuu wa wilaya ya Chato Dr. Eugen amewashukuru wadau hao kwa kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na rafiki katika mazingira yao lakini pia amewaomba wasikomee Mganza tu bali wafike na vituo vingine kwani nako wanamahitaji mengi kama ambavyo Mganza imesaidiwa na sasa inag'ara kwelikweli.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.