Soko la Samaki la Kasenda lipo katika kijiji cha Nyabugera Kata ya Mganza kilomita 37 kutoka Makao Makuu ya Wilaya , Soko hili ni la pili kwa ukubwa ukiacha soko la Kirumba lililopo jijini Mwanza, Soko lipo kando kando ya Ziwa victoria ambapo limetenganishwa na maji na kupakana na Hifadhi ya Taifa ya Rubondo wakati wote watalii wamekuwa wakipitia soko la samaki la kasenda kuelekea Hifadhini. Soko hili limekuwa likihudumia Ndani na Nje ya Nchi kama vile nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, DRC-Congo na nchi nyigine zinazotuzunguka.
UTAWALA
Soko la samaki la Kasenda lipo chini ya Halmashauri ya wilaya ya Chato na kusimamiwa na uongozi wa soko. Soko limekasimiwa kukusanya Tsh 140,000,000.00 kwa mwaka ambapo kufikia mwezi Disemba , 2018, makusanyo yalikuwa Tsh 31,160,180.00 sawa na asilimia 22.25 ya makisio ya mwaka.
Mhe: Balozi wa Japan nchini Tanzania,
Soko lina jumla ya wanachama 241, miongoni mwao, wanaume ni 164 na wanawake ni 77.
UJENZI NA UPANUZI WA SOKO LA SAMAKI LA KASENDA
Ujenzi wa soko hili unafadhiliwa na Ubalozi wa Japan Tanzania ambapo shughuli zinazofanyika ni ujenzi wa ghala kubwa la kuhifadhia samaki na kukarabati soko la zamani ili iweze kuwahudumia wafanyabiashara wa samaki na mazao mbalimbali kwenye mwalo wetu huu wa Kasenda.
Mradi wa ujenzi na utanuzi wa soko umegharamu kiasi cha Tsh 378, 378, 080.00 ambapo Ubalozi wa Japan Umetoa kiasi cha Tsh 320,958,450.00 bila VAT kwa ajili ya Kujenga ghala kubwa la kuhifadhi samaki/Dagaa na Kurekebisha Soko la zamani ambalo linatumika kuuzia samaki na bidhaa zingine kama mboga mboga na matunda. Halmashauri inalipa (VAT) ambao ni Tsh 57,419,630.00
Mkandarasi M/S DG GROUP OF COMPANIES LIMITED ya S. L. P 6269 MWANZA iliingia Mkataba No LGA/039/2016/2017/EJ/W/01 na HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO kwa ajili ya kazi ambapo mkataba ulianza rasmi tarehe 01/02/2017 na kumalizika tarehe 30/11/2017. Muda wa mkataba ulikuwa ni wa miezi 10.
Mpaka sasa kazi zote kuhusu Upanuzi na Ukarabati wa Soko la Samaki Kasenda zimeshakamilika.Kazi zilizofanyika kwa mujibu wa mkataba na makubaliano ni kama ifuatavyo;
FAIDA TARAJIWA KUTOKANA NA UJENZI NA UTANUZI WA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA LA KASENDA
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.