Wilaya inaendesha Shughuli za uvuvi katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 896 ndani ya ziwa Victoria. Aidha mkakati wa Wilaya kwa sasa ni kujielekeza katika uanzishaji wa mabwawa ya kufuga samaki kwenye maeneo ya kando kando ya ziwa, mito mikubwa na mabonde ya mpunga yenye uwezo wa kupata maji ya kutosha.
Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Wilayani Chato, unatumia Mfumo Shirikishi Jamii kupitia Vikundi vya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Mwaloni (BMUs) ambapo kwa sasa Wilaya inazo BMU 24 na mialo rasmi 36, soko moja la Kimataifa Kasenda na Mwalo mmoja uliojengwa kijiji cha Kikumbaitale.
Masoko yanayochukua samaki hawa ni pamoja na viwanda vya kusindika samaki vya Mwanza, Musoma na Bukoba; masoko ya ndani ya Wilaya ni Kasenda, Bwanga, Buseresere, Buziku, Chato na Kasenga; masoko ya nje ya Wilaya ni kama Geita, Kahama, Runzewe, Bukoba, Biharamulo, Ngara, Mwanza, Kigoma, Dar es salaam, Dodoma, Shinyanga, Arusha na masoko ya nje ya nchi ni Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia na Malawi.
Wilaya ina jumla ya wavuvi 3,336 kati yao, Wavuvi 3110, wanatumia vyombo vya uvuvi wengine wanatumia njia mbalimbali za asili.
Ufugaji wa samaki umeimarishwa zaidi kama njia mbadala ya kuongeza uzalishaji na kupunguza utegemezi wa samaki toka ziwani peke yake. Kwa sasa Wilaya inacho kituo 1 cha kuzalisha Vifaranga kilichopo kata ya Nyamirembe na Mabwawa 163 ya ufugaji wa samaki yaliyopo maeneo mbalimbali ndani ya wilaya.
Wilaya inaendelea na juhudi za kudhibiti uharibifu wa mazingira na uvuvi haramu kwa kutumia dhana shirikishi jamii kati ya Maafisa Uvuvi, Polisi, Vikundi vya Kusimamia Rasilimali ya Uvuvi Mwaloni (BMU) na Wenyeviti wa Vijiji.
Katika kutunza mazingira, vikundi vya BMU vimehamasishwa kufunga maeneo ya mazalia na makulio ya samaki kipindi cha mwezi Januari hadi Juni ya kila mwaka na Uvuvi haramu umeendelea kupigwa vita kupitia doria. Magari, mitumbwi na masoko ya samaki yameendelea kufanyiwa ukaguzi wa kushitukiza kwa lengo la kukamata samaki wachanga.
Kuanzia mwezi Januari hadi Desemba, 2017 Wilaya imefanikiwa kukamata nyavu haramu aina ya Timba 2,770 zenye thamani ya Tsh.221,600,000/=, Kokoro 202 zenye thamani ya Tsh.202,000,000/= , Katuli 201 zenye thamani ya Tsh.402,000/=, nyavu ndogo za dagaa 99 zenye thamani ya Tsh.69,300,000/= , Tupatupa 45 zenye thamani ya Tsh.900,000/=, nyavu ndogo za makila 3,753 zenye thamani ya Tsh.18,765,000/= na mitumbwi 38 yenye thamani ya Tsh.11,400,000/= . Jumla ya nyavu 7,150 zenye thamani ya Tsh.525,207,000/= zimeteketezwa kwa moto.Kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini:-
Jedwali kuonesha takwimu za ukamataji wa nyavu haramu na thamani yake kuanzia mwezi Januari hadi Desemba, 2017;
Mwezi |
Kokoro
|
Timba
|
Nyavu ndogo za makila |
Katuli |
Madema |
Tupatupa |
Nyavu za dagaa chani ya kiwango |
Mitumbwi |
JANUARI |
4 |
70 |
112 |
- |
- |
- |
8 |
3 |
FEBRUARI |
15 |
114 |
360 |
14 |
- |
3 |
- |
6 |
MACHI |
5 |
150 |
475 |
6 |
- |
4 |
10 |
3 |
APRILI |
8 |
106 |
506 |
3 |
- |
2 |
2 |
7 |
MEI |
20 |
44 |
204 |
2 |
- |
5 |
1 |
- |
JUNI |
- |
78 |
125 |
13 |
- |
- |
3 |
- |
JULAI |
- |
644 |
151 |
- |
- |
- |
5 |
5 |
AGOSTI |
43 |
84 |
320 |
82 |
- |
- |
- |
6 |
SEPTEMBA |
28 |
74 |
116 |
32 |
- |
- |
6 |
- |
OKTOBA |
24 |
306 |
384 |
11 |
12 |
2 |
21 |
2 |
NOVEMBA |
46 |
802 |
650 |
30 |
16 |
29 |
35 |
6 |
DESEMBA |
19 |
298 |
350 |
8 |
14 |
- |
8 |
- |
Jumla |
202 |
2770 |
3753 |
201 |
42 |
45 |
99 |
38 |
Thamani |
202,000,000/= |
221,600,000/= |
18,765,000/= |
402,000/= |
840,000/= |
900,000/= |
69,300,000/= |
11,400,000/= |
HATUA ZILIZOCHUKULIWA DHIDI YA WAVUVI HARAMU
Kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka 2017 watuhumiwa 21 waliojihusisha na uvuvi haramu walifikishwa mahakamani ambapo jumla ya kesi 17 zilifunguliwa, katika kesi 4 watuhumiwa wamefungwa mwaka mmoja na miezi sita, kesi saba (7)watuhumiwa wamelipa faini na kesi sita (6) zinaendelea mahakamani.
MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UVUVI HARAMU
MAFANIKIO YALIYOPATIKANA BAADA YA HATUA ZA KUPAMBANA NA UVUVI HARAMU
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.