Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mhe Mwenyekiti wa Halmashauri na Baraza la Madiwani katika ukumbi wa Halmashauri ametoa taarifa ya mapokezi ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 9 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo toka Serikalini ikiwa ni utayari wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ni katika Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani kujadili taarifa Robo ya Tatu kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari hadi Machi
Aidha Mhe Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Christian Manunga akifungu mkutano huo nae ametoa kauli ya kumpongeza Mhe. Rais kwa namna ambavyo Serikali yake naendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta za Afya, Elimu na Maji, kauli ambayo imeungwa kwa asilimia 100 wahe. Madiwani katika mkutano huo wa Baraza.
Mhe Mkuu wa willaya ya Chato Eng Deusdedith Katwale akiongea na wajumbe wa Mkutano huo, wageni waalikwa na wananchi wote kwa ujumla waliofika katika mkutano huo kwa lengo la kufatilia na kusikiliza utendaji kazi wa Halmashauri kwa kipindi cha miezi 3 yaani kuanzia Januari hadi Machi 2023 amesisitiza kwa kusema,
" japo leo hapa mnashangila lakini niombe na wala sitegemei kuona fedha hizi eti zinarudi kisa tumeshindwa kutumia kwa wakati"
Lakini pia Mhe Katwale amewataka Wahe. Madiwani hakikisheni miradi hii inayotekelezwa katika maeneo inatekelezwa kwa viwango na ubora wa hali ya juu.
Aidha Mhe. Katwale amewapongeza wataalamu kwa namna ambavyo sasa wanaonyesha kubadirika katika utendaji kazi jambo ambalo linaleta tija kwa ustawi wa Halmashauri yetu.
Kwa upande wake Mhe. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya Ndg. Barnabas Nyerembe ameomba fedha hizo ambazo Serikali imetoa pamoja na kwenda kutekeleza miradi hiyo niombe pia ziende zikawanufaishe watu wetu ndani ya maeneo yetu, " ni aibu sana kuona mradi unatekelezwa mfano kata ya kachwamba lakini hata fundi ujenzi kwa njia ya force account anatoka Geita au Mwanza na hatoki katika maeneo ambayo mradi unatekelezwa, jambo hili halikubaliki na niseme wazi tabia hii iwe mwanzo na mwisho ndani ya wilaya yetu ya Chato"
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.