Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Ndg. Mandia H. Kihiyo, ameongoza timu ya Menejimenti ya Halmashauri hiyo kwenye ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji miradi ya maendeleo kwa lengo la kukagua hatua za miradi na utekelezaji wa maelekezo ya ziara zilizopita, kushauri / kutatua changamoto mbalimbali hususani zinazohitaji utaalamu, kujiridhisha ubora na thamani ya fedha katika miradi, huku likikaziwa suala la ukamilishaji wa haraka ili itumike na kuwanufaisha wananchi kwa wakati kutimiza lengo la Serikali.
Ziara hiyo imefanyika Julai 31, 2025 ambapo imebaini kuwa miradi mingi imefikia hatua nzuri sana na inaridhisha kwa kiwango kikubwa lakini pia imeonekana kuwa maelekezo na ushauri uliotolewa na wataalamu ziara zilizopita baada ya kukuta mapungufu machache umetekelezwa na kupelekea majengo kuwa imara na ubora unaoendana na maelekezo ya Serikali.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo Ndg. Kihiyo ameipongeza Serikali kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo hususani huduma za afya zimeboreshwa kuanzia miundo mbinu, vifaa tiba pamoja na wataalamu kuongezwa hali kadhalika upande wa elimu bila kusahau maji yanapatikana kila mahali, umeme, na barabara zinazopitika kurahisisha biashara na kukuza uchumi huku akisisitiza wananchi kuilinda miundo mbinu hiyo ili iweze kudumu lakini pia kuenzi juhudi za Serikali.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.