Leo Julai 31, 2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Chato, Mkoani Geita ametoa zawadi za vyeti vya pongezi kwa Waganga Wafawidhi wa Vituo vya Afya, Zahanati pamoja na Hospital ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao katika ufanyaji kazi na utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Zawadi hizo zimetolewa kwa Vituo vya Afya vinne (4) ambavyo ni Butarama kipengere cha Mnyororo wa Ugavi (Supply Chain ELMIS Data), Iparamasa kipengere cha Usafi wa Mazingira, Bwanga kipengere cha Usimikaji na Matumizi ya GOT- HOMIS na Muganza kipengere cha Ukusanyaji wa Mapato yatokanayo na Huduma za Afya.
Kwa upande wa Zahanati ni vituo nane (8) tu vilivyopata zawadi hiyo ambavyo ni Nyamirembe na Ihanga kipengere cha Mnyororo wa Ugavi (Supply Chain EL-MIS Data), Bupandwampuli kipengere cha Usafi wa Mazingira na Buseresere kipengere cha Usimikaji na Matumizi ya GOT-HOMIS, Zahanati za Buseresere na Makurugusi kipengere cha Ukusanyaji wa Mapato yatokanayo na Huduma za Afya nana mwisho ametoa zawadi Hospitali ya Wilaya kipengere cha Usafi wa Mazingira na Usimikaji na Matumizi ya mfumo wa GOT-HOMIS.
Akitoa zawadi hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Mandia Kihiyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri amewataka Waganga Wafawidhi, Wauguzi, Wahasibu na Makatibu wa Afya amewataka kila mmoja kwenda kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maadili ya kazi na Utu wa Mtu, kusimamia Miradi ya Maendeleo kwa uadilifu na ubora unaotakiwa.
Aidha Ndg. Mandia amewataka Waganga na Wauguzi Wafawidhi kuhakukisha wanasimamia na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga.
Akihitimisha Ndg. Mandia amewaasa Watumishi wote wa Umma kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa Amani na Utulivu huku akiwataka kutojihusisha na vitendo vinavyoweza kusababisha vurugu au kuondoa Amani ya Taifa letu.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya ya Chato Dkt. Daniel Mzee amemhakikishia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuwa yeye pamoja na timu yake wamejipanga vizuri kuhakikisha maelekezo pamoja na maagizo yote aliyoyatoa yanakwenda kutekelezwa kwa ukamilifu na ubora.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.