Zaidi ya wananchi 15,000 wa kata ya Bukome wilayani Chato wameanza kunufaika na ujenzi wa kituo cha kata hiyo kilichojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa gharama ya shilingi 1,052,000,000/=.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mandia Kihiyo amesema kukamilika kwa kituo hicho kutasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Wilaya iliyopo mjini Chato.
“Kituo hiki kimepanuliwa, hapo awali ilikuwa ni zahanati ya kijiji cha Nyabilezi kwa sasa ni kituo cha Afya cha kata ya Bukome, tumeamua kujenga kituo hiki ili kuwasogezea wananchi wa kata hii huduma za Afya ambapo hapo awali walikuwa wanalazimika kwenda Chato kupata huduma za Afya” alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Diwani wa kata ya Bukome Mhe. Petro Kilasa amesema kukamilika kwa kituo hicho kumesaidia kuokoa maisha ya wakazi wa kata ya Bukome ambao hapo awali walikuwa wanafuata baadhi ya huduma katika hospitali ya Wilaya ya Chato kwa zaidi ya umbali wa kilometa 20 lakini hivi sasa wananchi hao wataweza kupata huduma hizo katika eneo lao.
Mhe. Kilasa Amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kujenga kituo cha Afya katika kata hiyo kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kunusuru maisha ya wananchi wa kata ya Bukome ambao wamekuwa wakililia kituo hicho kwa muda mrefu.
Juma Bunzali (56) ambeye pia ni mwananchi wa kijiji cha Nyabilezi amesema kukamilika kwa kituo hicho cha Afya cha kata ya Bukome kutapunguza gharama za usafiri na usumbufu wa kutafuta matibabu hasa kwa wale waliozoea kufuata huduma katika hospitali ya wilaya ya Chato.
“Zamani tulikuwa tunakuja hapa baadhi ya vipimo tulilazimika kwenda hospitali ya Wilaya ya Chato lakini kwa sasa vipimo vyote vinapatikana hapahapa tena ndani ya muda mfupi tu” alesema Bwana Bunzali.
Kituo cha Afya cha kata ya Bukome kimejengwa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wan je (OPD), Jengo la akina mama, jengop la upasuaji, Maabara, jengo la maiti, na nyumba moja ya watumishi wawili ambapo jula ya shilingi 730,000,000/= zilitumika.
Awamu ya pili ilihusisha ujeniz wa uzio wa kituo hicho, njia za kutembelea, matundu 6 ya vyoo, jengo la kufulia nguo na nyumba moja ya watumishi watatu ambapo jumla ya shilingi 322,000,000/ zimetumika na kufanya kituo hicho kugharimu shilingi milioni 1,052,000,000/= kukamilika kwake
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.