Uzinduzi wa gereza jipya la Wilaya ya Chato kupunguza gharana za usafirishaji na msongamano wa waalifu katika magereza mengine ambayo yalikuwa yakihifadhi waalifu.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua wa Gereza jipya la Wilaya ya Chato Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa katika Wilaya ya Chato kumekuwa na changamoto ya kutokuwa na Gereza na kulazimika kupeleka waalifu katika Gereza la Biharamulo hivyo gereza hilo litapunguza gharama za usafirishaji wa waalifu ambao wa walikuwa wakipelekwa magereza ya mbali ili kuhifadhiwa.
Ameongeza kuwa ujenzi wa Gereza hili utasaidia kuendeshwa kwa mashitaka kwa kufuata ratiba kwa kuwa wakati mwingine ratiba zinaingiliana lakini pia changamoto za magari, mafuta na umbali zilikuwa kikwazo kikubwa katika uendeshaji wa mashitaka hivyo kusababisha watu wenye matatizo mbalimbali kuendelea kushikiliwa katika magereza kwa muda mrefu huku akikosa haki zake hata kama hana hatia.
Aidha, mheshimiwa Dkt Mwigulu nchemba ametoa rai kwa maafisa na askari wa gereza kuhakikisha wanatunza majengo na miundombinu ya gereza hilo na kufanya kazi kwa uadilifu ili maadili yaliyowekwa katika magerezani yanazingatiwa '' licha ya kazi nzuri inayofanywa na viongozi walio wengii zipo taarifa kwenye baadhi ya magereza watumishi hawazingatii maadili ya kazi kwa kuwa wengine wamekuwa wakiwapa waalifu simu bila kujua wanafanya mawasiliano na watu wa namna gani vitendo hivi vina hatarisha usalama wa gereza na askari pia''.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amelitaka jeshi la magereza kupitia gereza la Wilaya ya Chato ambalo limejengwa kijiji cha Nyangomango kutumia maeneo yaliyopo na watakayopewa na Mkoa kuzalisha mazao mbalimbali ya kilimo na mifugo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Mkoa na taifa.Ameongeza kuwa jeshi la magereza limejijengea heshima kubwa nchini kwa kuzalisha vifaa bora kama vile samani za nyumbani na ofisini, viatu hivyo jeshi linaweza kuleta mapinduzi ya kimkakati ya kiuchumi.
Naye Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera Nehemia Nkondo ameeleza katika taarifa kuwa ujenzi wa Gereza la Chato ulianza mwaka 2011 katika kijiji cha Nyangomango kwa kupata hekari 50 kutoka kwa wananchi ambapo serikali ilitoa zaidi ya Shilingi bilioni 1.5 mpaka sasa mradi umetumia kiasi cha shilingi milioni 613.6 sawa na asilimia 40%. kiasi cha Shilingi milioni 903.6 zinaendelea kutumika ambapo kuna ujenzi wa mabweni 4 ya wafungwa yenye uwezo wa kuhifadhi wafungwa 50 kila moja, uvutaji wa maji na ujenzi wa mabweni 2 ya wanawake.Kazi zinazoendelea ni ujenzi wa jengo la utawala, nyumba za watumishi.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.