Halimashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita kupitia kikao cha Baraza la Madiwani imemuagiza Afisa Kilimo Mifugo na Uvuvi katika halimashauri hiyo kuhamasisha kilimo kinachoendana na mabadiriko ya hali ya hewa kama njia ya kuimarisha usalama wa chakula kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Christian Manunga amesema wananchi hususani wakulima wa wilaya hiyo wamekua wakishindwa kulima mazao yanayoendana na hali ya hewa na kwamba ni jukumu la idara ya kilimo kuhakikisha inawajengea uwezo wakulima ili waweze kuzarisha kwa tija.
Manunga amesema hategemei kuona mkulima yeyote wa wilaya ya Chato akipata mavuno hafifi kwa sababu ya changamoto za mabadiriko ya hali ya hewa na badala yake maafisa ugani waendeshe mashamba darasa kwa wakulima ikiwa ni pamoja na kuwashauri juu ya aina ya mazao wanayotakiwa kuzarisha kulingana na jografia ya maeneo yao.
Nae afisa kilimo mifugo na uvuvi katika halimashauri ya wilaya ya Chato Jerad Ismail Mgoba amesema tayari amekwisha waagiza maafisa ugani wa vijiji na kata kuendesha mafunzo kwa wakulima kupitia mashamba darasa juu ya namna bora za kukabiliana na mabadiriko ya hali ya hewa kwa kulima mazao ya muda mfupi na kwamba zoezi la kuelimisha na kuhamasisha wakulima ni endelevu.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.