Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato amekanusha vikali uvumi uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa standi kuu ya mabasi ya Chato "Kahumo bus terminal" imetelekezwa na kubaki magofu.
Uvumi huo ambao umezua taharuki kwa baadhi ya wananchi,umelenga kudhoofisha jitihada kubwa na nzuri za serikali kusogeza huduma kwa wananchi wa wilaya ya Chato ikiwemo mikoa jirani ya Kagera,Kigoma,Shinyanga,Mwanza na Musoma.
Akizungumza na mwandishi wetu,Mkuu wa wilaya ya Chato,Deusdedith Katwale,amewataka wananchi kupuuza uvumi huo kwa kuwa unalenga kupotosha jamii na kwamba serikali ya awamu ya sita inaendelea na ujenzi wa stendi hiyo kwa maslahi mapana ya jamii.
"Kuna baadhi ya watu wasioitakia mema wilaya ya Chato...wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kueneza propaganda za uongo mitandaoni...baadhi yao wanasema stendi ya imebaki magofu wengine wanasema uwanja wa ndege haufanyi kazi...mimi niwahakikishie kuwa miradi yote ya Chato inaendelea vyema na ina manufaa makubwa sana kwa jamii"
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato, Mandia Kihiyo, amesema ujenzi wa stendi hiyo umefikia aslimia 95 na kwamba unatarajiwa kukamilika juni 2023.
Hata hivyo anasema zaidi ya mabasi makubwa 39, Costa 19 na Hiace 78 zinatumia stendi hiyo kwa kila siku huku baadhi ya mabasi kutoka nchi jirani ya Uganda yakisafirisha abiria kuelekea jijini Mwanza.
Kadhalika vijana machinga,waendesha boda boda na bajaji pia wanajipatia riziki kwa kusafirisha abiria wanaoshuka na kwenda chato mjini.
"Niwaombe wananchi wasikubali kupotoshwa...stendi yetu imegawanyika pande mbili stendi ndogo inatumika na kubwa tunatarajia kuanza hivi karibuni..hivyo wananchi wajiandae kuomba vibanda vya kufanyia biashara mbalimbali...pia tunazo kumbi za kisasa ambazo zitatumika mara tu ujenzi utakapo kamilika" amesema Kihiyo.
Ujenzi wa stendi ya kisasa ya Kahumo umeanza kutekelezwa mwaka 2020 kwa mpango wa miradi ya kimkakati ambapo kukamilika kwake kunatarajiwa kuinufaisha jamii kwa kurahisisha upatikanaji wa usafiri,kuongeza ajira na kuinua uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla.
Mwisho.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.