Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Edwin Rutageruka akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakulima na wasindikaji wa bidhaa za kilimo Wilayani Chato
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri Semeon akifungua mafunzo ya siku nne ya wakulima na wasindikaji wa bidhaa za kiloimo kutoka Chato.
Mgeni Rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wakulima na wasindikaji wa Bidhaa za kilimo Mku wa Wilaya ya Chato akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wasindikaji wa bidhaa za kilimo
Mgeni Rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wakulima na wasindikaji wa Bidhaa za kilimo Mku wa Wilaya ya Chato akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakulima wa kata ya Muungano
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa wakimsilikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo
Kutokana na Halmashauri ya Wilaya ya Chato kuwa na wazalishaji wengi wa bidhaa za kilimo husasan zao la Alizeti, Mamlaka ya Taifa Biashara Tanzania (TANTRADE) imevutiwa na wazalishaji hao kutoka Chato na kuahidi kutoa ushirikiano ili kuboresha mazingira ya wazalishaji hao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Taifa ya Biashara Edwin Rutageruka amesema kutokana na Wilaya ya Chato kuwa na wazalishaji wengi wa mazao ya biashara, chakula pamoja na wasindikaji wa bidhaa za kilimo wameona washirikiane na uongozi wa Halmshauri kuandaa mafunzo maalumu kwa wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa za kilimo wilayani Chato
“Baada ya kuona jitihada hizi tukaomba tuweze kufanya mafunzo maalumu kwa wazalishaji hawa… tumeona tuanze elimu ya mbegu, vifungashio, vipimo pamoja na ubora wa bidhaa mnazozalisha” aliongeza Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE.
Amesema kutokana na Mafuta ya Alzeti kuwa bora zaidi wameamua kuwaalika wazalishaji wa Mafuta ya Alizeti kutoka Chato washiriki kwenye maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yatakayofanyika kwenye viwanja vya maonesho ya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 5 hadi 9 Septemba 2018.
Mkurugenzi Mkuu pia ameahidi kutoa banda kwa Wilaya ya Chato kwenye maonesho ya kibiashara ya Kimataifa Sabasabakwa mwaka 2019 ili wazalishaji wa mafuta ya Alzeti kutoka Chato waweze kuonesha bidhaa hiyo.
Mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri Semeon ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita amesema mafunzo hayo ni lazima yalenge kuongeza tija kwenye upatikanaji wa mbegu bora, uzingatiaji wa kanuni bora za kilimo cha zao la Alzeti pamoja na kusindika Alizeti kwa viwango vinavyoubalika ndiyo maana wadau wote walialikwa ili kutoa mafunzo kwa wakulima na wazalishaji hao.
Mkuu wa Wilaya amesema ili kuzalisha bidhaa bora zaidi Wilaya iko tayari kutoa eneo kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa mbegu bora ya zao la Alizeti, hivyo amewaomba wakala wa mbegu wa Taifa kusaidia jambo hilo ambapo amesema kutasaidia kupunguza bei ya mbegu hizo na hatimaye kuwa na wakulima wengi wa zao la Alzeti.
Mafunzo haya ya siku nne yamendaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa kushirikiana na Mamlaka ya Taifa ya Biashara ambapo pia wameshirikishwa wadau wengine ambao ni Wakala wa Mbegu wa Taifa, Wakala wa Vipimo pamoja, Mamlaka ya Chakula na dawa na SIDO yanafanyika kwenye ukumbi wa Mshikamano SACCOS uliopo Chato.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.