Pongezi hizo zimebainishwa leo na wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango katika ziara iliyofanyika mapema hii leo ambapo kamati hiyo ilipata fursa ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Stand ya Mabasi Makubwa ya mikoani katika Stand Kuu ya Kahumo ndani ya Halmashauri ya Chato.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato Mhe. Christian Manunga yeye amewataka wataalamu wa Halmashauri kufanya kazi kama timu na siyo kila siku kukombana ameongeza kwa kusema, " hakika leo mmenifurahisha kwani miradi tuliyotembelea inavutia na sasa inaonyesha mmeanza kutuelewa niombe tu msirudi nyuma chapeni kazi"
Wakichangia Wahe.Madiwani katika nyakati tofauti hawakusita kutoa pongezi zao za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo pamoja na timu yake ya Menejimenti kwani kazi kweli inaonekana na kupendeza si kwamacho tu hata ubora wake.
Kwa upande wake Ndg. Mandia Kihiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato amewashukuru Wahe. Madiwani kwa kuona na kuthamini kile ambacho wataalamu wake pamoja na menejimenti kwa ujumla inafanya, huku akiahidi kufanyia kazi ushauri na maoni yote waliyoyatoa ikiwa ni katika kuhakikisha Chato inaendelea kufanya vizuri siku zote.
Mkuu wa Idara ya Mipango na Ufatiliaji Chato Ndg. Mhenziwa Bundala ameahidi kuendelea kusimamia miradi yote kwa ukaribu kushirikiana na idara na vitengo venye miardi hiyo ili iweze kuleta tija kwa wanachato na taifa kwa ujumla .
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.