• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Malalamiko |
    • Staff Mail |
Chato District Council
Chato District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chato

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Kilimo
      • Eduction
        • Primary
        • Secondary
      • Fedha
      • Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
      • Water
      • Works
      • Afya
      • Ardhi, na Maliasili
    • Vitengo
      • Procurement
      • ICT
      • Internal Audit
      • Legal
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uchimbaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Vivutio Vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Health Service
    • Education Service
    • Water Service
    • Agriculture Activities
    • Livestock Activities
    • Fisheries Activities
  • Councilors
    • Councilors List
    • Standing Committee
      • Finance, Planning & Administration
      • Education, Health & Water
      • Environment, Works & Economic
      • HIV/AIDS Control
      • Ethics
    • Schedule
      • Councilors Meting Schedule
      • Meet with Councilor
  • Miradi
    • Planned Projects
    • Miradi inayoendelea Kutekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Repoti
    • By Law
    • Fomu
    • Strategic Plan
    • Huduma ya Mkataba kwa Mteja
    • News Paper
  • Kituo vya Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Matukio
      • Habari

WAZIRI ATENGUA KITENDAWILI CHA SOKO LA KASENDA

Posted on: December 13th, 2021


Waziri wa mifugo na Uvuvi mhe. Mashimba  Ndaki amesema serikali ya Tanzania bado inalitambua soko kuu la kimataifa la Kasenda kuwa ni miongoni mwa masoko matatu ya kimataifa ambayo yanatumika kutoa vibali ili kuhakikisha mazao ya samaki yanayopelekwa katika mataifa mengine yanakuwa katika ubora wa hali ya juu.


Waziri Ndaki ameyasema hayo leo tarehe 13.12.2021 wakati wa ziara yake ya kuongea na wananchi na wafanya biashara katika soko la kimataifa la Kasenda lililopo kata ya Muganza wilayani hapa.

"Tanzania tuna masoko matatu tu ya kimataifa, soko la samaki la Feri lililopo Dar es Salaam, Soko la Kirumba lilolopo jijini Mwanza na Kasenda lililopo Chato. Nataka niwahakikishie soko lenu la Kasenda lipo  pale pale na lipo kimkakati chini ya Wizara ya Mifugo na uvuvi, halikuletwa hapa kwa bahati mbaya" alisema mhe. Waziri Ndaki.


Waziri Ndaki amesema masoko mengine yanayotajwa na baadhi ya watu hayapo na Wizara haiyatambui kwani masoko hayo matatu yanalindwa na miongozo pamoja na mindombinu ambayo serikali imewekeza katika masoko hayo.


Waziri Ndaki amesema kwa mwaka 2020/2021serikali kupitia Wizara imeweza kukusanya mapato ya zaidi ya shilingi bilioni mbili  kutoka katika soko  la Kasenda

"kwenye soko hili tumewekeza fedha nyingi, tunao watumishi pia wa Wizara hapa zaidi ya watano kwa hiyo lazima tulilinde" alisisisitiza Mhe. Waziri Ndaki.


Aidha Waziri Ndaki ameonya tabia ya baadhi ya viongozi kuwabughuzi wafanya biashara kwa kuwataka wakate leseni za uvuvi katika maeneo wanayofanyia shughuli za uvuvi hivyo amesema wafanya biashara watatumia leseni zao bila kujali leseni imekatwa wapi, "sasa hivi hata ukikata leseni ya uvuvi ukiwa mkoa wa Mara unaweza ukafanya shughuli za uvuvi hata ukiwa Chato, hakuna tatizo kabisa..kuwalazimisha wafanyabiashara kukata leseni za uvuvi kila wilaya kitendo hiki ni kinyume na sheria zetu na kufanya hivyo ni kinyume na sheria" alisistiza Waziri Ndaki.



Mapema akimkaribisha Waziri Ndaki Mbunge wa jimbo la Chato mhe.Medard Kalemani amesema wafanyabishara wa dagaa wanaotumia soko la Kasenda kwa sasa wameathirika sana kutokana na kauli za baadhi ya viongozi kuwazuia wafanyabiashara hao kupitishia mizigo yao kwenye soko la Kasenda ambapo amesema kutokana na madhara hayo hivi sasa soko hilo linao wafanyabishara 10 tu waliobaki katika soko hilo ambapo hapo awali zaidi ya watu 13,000 walinufaika na soko hilo.


Mhe. Kalemani pia amesema hapo awali soko hilo liliweza kuingiza mapato kiasi cha shilingi milioni 14 kwa siku lakini hivi sasa mapato yanaishia shilingi laki 8  kwa siku ambapo zaidi ya tani 30 za dagaa ziliipitia katika soko hilo lakini kwa sasa dagaa dagaa wamepungua sana.


Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mhe. Bathromew Manunga amesema soko la Kasenda kwa sasa kumekuwa likiingiliwa na  kauli za baadhi ya viongozi kutoka Wilaya jirani ambazo zinawachanganya wafanyabishara na kusababisha baadhi ya wananchi wa Kasenda kutaka kujichukulia sheria mkononi kwa kukasirishwa na kauli za viongozi kutoka Wilaya jirani juu ya matumizi ya soko hilo la Kasenda.

Matangazo

  • MATOKEO YA UDEREVA CHATO DC September 27, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI CHATO DC September 20, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI CHATO May 24, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI CHATO July 19, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MSINGI WA MAENDELEO NI LAZIMA UTOKANE NA WANANCHI WENYEWE

    April 26, 2025
  • WADAU CHATO WATHIBITISHA MCHAKATO WA KUGAWANYA JIMBO UMEFATA TARATIBU ZOTE ZA VIKAO MBELE YA TUME HURU YA UCHAGUZI

    May 24, 2025
  • MILIONI 431.2 ZAWAGUSA WANANCHI SEKTA YA MAJI CHATO

    April 16, 2025
  • WANANCHI WA KINSABE WAISHUKURU RUWASA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI YA BOMBA

    April 16, 2025
  • View All

Video

MHE. NDEJEMBI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUWA NA NIDHAMU NA KUTIMIZA WAJIBU KWA WELEDI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HOTUBA YA BAJETI TAMISEMI 2019
  • Mwongozo wa Matumizi Bora na Salama wa Vifaa vya TEHAMA
  • MWONGOZO WA KUSIMAMIA NA KUENDESHA TOVUTI ZA SERIKALI
  • MWONGOZO WA OPRAS
  • TAARIFA KWA UMMA UFUNGUZI WA JENGO JIPYA JIPYA CRDB

Tovuti Linganifu

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais- TAMISEMI
  • eMrejesho - Malalamiko/taarifa yeyote kutoka kwa wananchi,Watumishi wa Umma/Wastaafu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Ofisi ya Rais- Utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI

    Postal Address: 116 CHATO

    Telephone: +255282228007

    Mobile:

    Barua pepe: ded@chatodc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Malalamiko
    • map
    • Service

Copyright©2016 CDC . All rights reserved.