Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa zao la pamba nchini wasikubali kuuza pamba yao chini ya bei elekezi ya shilngi 1200 kwa kilo.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amewashauri wafanyabiashara wa zao hilo waungane na kuanzisha viwanda vya kutengeneza nyuzi na nguo ili kuongeza thamani ya zao hilo kabla ya kuuza.
Waziri Mkuu ameyasema hayo siku ya Jumamosi tarehe 21 Septemba wakati akiongea na wananchi pamoja na viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika Chato (CCU) kwenye kiwanda cha kuchambua pamba kilichoko mjini Chato.
“Hata mkiwa na shida msikubali kuuza pamba yenu chini ya shilingi 1,200 kwa kuwa haitachukua muda mrefu mtakuwa mmeshapata fedha zenu, tuna taarifa kuwa kuna wanunuzi wamepata fedha na wanatumia watu kwenda kuwalaghai wakulima kwa kutaka kununua pamba kwa bei ya shilingi 800, msikubali na mkiwaona mtupe taarifa.”
Waziri Mku pia aemesema kama viwanda vya nyuzi vikijengwa nchini vitakuwa na soko la uhakika kutokana na hivi sasa kutokuwa na viwanda hivyo ambapo serikalai amewahahakikishia mazingira mazuri kwa watanzania wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta hiyo kutokana na mahitaji hayo kuwa makubwa.
Meneja wa CCU Charles Nyasi alimwambia Waziri Mkuu kuwa kampuni za METL, KCCL na FRESHO zimejitokeza kununua pamba kupitia AMCOS na tayari kilo 9,611,860 zimenunuliwa kati ya kilo 11,140,529.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.